Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 12:03

Wanawake Kufanya Mgomo wa Mapenzi Kenya


Makundi hayo ya wanawake nchini Kenya yanasema yatasusia kufanya mapenzi na waume zao kwa muda wa siku saba, kama njia pekee ya kulinusuru taifa hilo na machafuko ya kisiasa.

Makundi hayo yanatoa wito kwa wanawake wote nchini Kenya kususia mapenzi na waume zao kwa muda wa siku saba, kuwashinikiza wanasiasa wa nchi hiyo, hususan Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga kuiepusha nchi hiyo na vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Katika kufanikisha mpango huo, wanawake hao wamewataka mke wa Rais Kibaki, Luci Kibaki na mke wa Waziri Mkuu Odinga, Aida Odinga kuzingatia hatua hiyo kwa kuwanyima mapenzi waume zao, hadi pale watakapo kuwa wamekomesha mivutano ya kisiasa.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG