Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:32

Tume Yachunguza Milipuko ya MabomuTanzania


Kufuatia milipuko ya mabomu iliyotokea Jumatano kwenye kambi ya Jeshi kwenye ghala la kuhifadhia silaha huko Mbagala Dar es salaam Tanzania, rais wa nchi hiyo Jakaya Kikwete alitembelea eneo hilo kujionea hali halisi akizungumza na sauti ya Amerika naibu waziri wa ulinzi Dr.Emanuel Nchimbi ameeleza kuwa kwa utaratibu wa jeshi la Tanzania na kwa mujibu wa sheria ya ulinzi wa taifa hilo baada ya tukio kama hilo linaundwa baraza la uchunguzi ambalo ndilo litatoa taarifa rasmi nini kilichotokea.Akizungumzia kuhusu eneo hilo amedai kuwa limedhibitiwa na wataalam wa mabomu ambao wanakusanya risasi na mabomu yaliyoenea sehemu mbalimbali na wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wa eneo hilo.Aidha aliongeza kuwa eneo hilo bado lina joto jingi na wananchi wa eneo hilo wasiwe na wasiwasi kwani limedhibitiwa na hawatarajii milipuko mingine alipoulizwa kuhusu uwezekano wa makosa ya kijeshi waziri huyo alisema wakati kambi hiyo ilipojengwa eneo hilo halikuwa na makazi ya raia kwani makazi hayo yameendelea kukua kadri mji unavyokua lakini akasema hiyo itakuwa ni sehemu ya matokeo ya uchunguzi.Mpaka hivi sasa idadi ya vifo imeripotiwa kuongezeka na kufikia watu 11. Alipojibu swali kuhusu operesheni za kijeshi kuathiriwa na milipuko hiyo waziri huyo alidai hiyo haiwezi kuathiri operesheni za kimataifa nchi hiyo inazoshiriki kama vile huko Darfur kwani silaha ziko salama chini ya uthibiti wa wataalam wa kijeshi.

XS
SM
MD
LG