Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 07:55

Milipuko ya Mabomu Yaitikisa Dar


Ghala ya silaha za kijeshi nje ya jiji la Dar es Salaam lililipuka na kusababisha moto mkubwa na taharuku katika mji mkuu huo wa biashara nchini Tanzania.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika, Dinah Chahali aliyepo jijini Dar es Salaam aliripoti kuwa majeruhi 24 wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, 11 katika hospitali ya Temeke, na wengine 9 katika hospitali ya jeshi la polisi barabara ya Kilwa.

Maofisa wa hospitali wanasema kuwa idadi ya majeruhi huenda ikaongezeka kwani majeruhi zaidi walikuwa wakiendelea kufikishwa hospitalini hapo.

Wakuu wa usalama waliwataka wananchi wawe watulivu na kufuata maelekezo ya kitaalamu kwa lengo la kurejesha hali ya utulivu na usalama.

Mwandishi wa Times FM jijini hapo, Sheiza Daudi alisema kuwa miongoni mwa watu waliopoteza maisha katika tukio hilo ni mtoto mdogo. Bwana Daudi alisema baadhi ya watu walijeruhiwa baada ya kugongwa na magari wakati wakijaribu kuvuka barabara.


XS
SM
MD
LG