Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 30, 2020 Local time: 07:27

Kikao cha Bunge Chaahirishwa Kenya


Mgogoro wa kisiasa kati ya Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka na Waziri Mkuu Raila Odinga umesababisha kikao cha kawaida cha bunge nchini Kenya kuahirishwa hadi wiki ijayo kwa matumaini kuwa mgogoro huo utakuwa umepatiwa ufumbuzi.

Mchambuzi wa siasa, Michael Tiampati anasema kiini cha mgogoro wa Kenya na hali ya kutokuelewana ndani ya serikali ya mseto ni uchu wa madaraka walionao baadhi ya viongozi wa Kenya.

Tiampati anasema kila upande unadai kuwa na mamlaka zaidi. Kwa upande wake chama cha ODM kinadai kuwa kinawajumbe wengi bungeni, huku chama cha PNU kikidai kuwa rais na makamu wake wanatoka chama hicho.

Anasema kuwa mvutano huo kati ya viongozi wa ODM na PNU umekwamisha mambo mengi ambayo yangeweza kufanyika kwa manufaa ya taifa, ikiwa ni pamoja na yale yote yaliyokubaliwa wakati wa utiaji saini mkataba wa kushirikiana madaraka uliosimamiwa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan.

Zinazohusiana

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG