Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 12:31

Serikali Yachunguza Mauaji Kenya


Rais Mwai Kibaki wa Kenya ameamru uchunguzi wa kina ufanywe kujua chanzo cha mauaji hayo yaliyohusisha vijana wenye hasira na watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa kundi lililopigwa marufuku nchini humo Mungiki.

Waziri Mkuu Raila Odinga na Waziri wa Usalama wa Taifa George Saitoti, walitembelea eneo la mlima Kenya na kuwashauri wakazi wa eneo hilo wadumishe amani.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika aliyepo nchini Kenya aliwakariri majeruhi waliolazwa hospitali kwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika machafuko hayo, wakisema kuwa mapigano yalikuwa yameandaliwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Ripoti zinasema kundi la vijana waliojikusanya kukabiliana na kundi la Mungiki, waliua wafuasi 14 wa kundi hilo baada ya maafisa wa polisi kusema kuwa wameshindwa kukabiliana na uhasama wa wahalifu.

XS
SM
MD
LG