Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 19:58

Amng'ata Nyoka Kuokoa Maisha Yake


Akiongea na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu kutoka Kenya, Bernard Nyaombe alisema Alhamisi kuwa alikutana na mkasa huo wa kutisha Jumapili majira ya saa moja wakati alipokuwa akijiandaa kupata chakula cha jioni.

Kitu ambacho hakujua ni kuwa nyoka mkubwa aina ya chatu, alikuwa alikuwa akikusudia pia kufanya kitoweo. Nyaombe anasema kuwa alimkanyaga nyoka huyo na mguu wake wa kushoto, na mara ghafla nyoka huyo alikuwa amejiviringisha kwenye mguu huo akijaribu kumdondosha chini.

Alitumia mbinu zote kujaribu kuokoa maisha yake lakini nyoka huyo alikuwa na nguvu kupita kiasi na nia ya kumuua. Nyaombe alisema, "Nilijaribu kupanua miguu, ili asinishike huu mguu mwingine, sasa ninaangalia hivi, nikashitukia ni python."

Alijaribu kutumia mikono kumkunjua kwenye mguu wake, lakini mkono nao ukanaswa. Mapambano yaliendelea kwa muda wa saa kadhaa na hatimaye nyoka aliamua kumpandisha juu ya mti, pengine kwa mategemeo kuwa binadamu hawana ujanja juu ya mti.

Lakini Nyaombe hakuwa tayari kupoteza maisha kwa urahisi. Alikusanya nguvu na kumng'ata meno huyo nyoka, uamuzi ambao anasema ulisaidia kuyaokoa maisha yake.

Sikiliza mahojiano na Nyaombe akielezea mkasa mzima wa tukio hilo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG