Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 18, 2021 Local time: 10:00

Mvutano wa Kisiasa Kenya


Kufuatia mvutano huo kati ya Rais Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan ambaye alisaidia juhudi za kuleta amani nchini Kenya alilazimika kuwasiliana moja kwa moja na viongozi hao wawili wa Kenya.

Taarifa zinasema kuwa Dokta Annan alilazimika kuwakumbusha Rais Kibaki na Bwana Odinga kuhusu umuhimu wa umoja na ushirikiano kati yao kwa manufaa ya taifa.

Siku chache zilizopita, Bwana Odinga alisema hadharani kuwa Rais Kibaki alikuwa ameanza kukiuka makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya mseto, na kwamba kibaki amekuwa akifanyakazi kienyeji kama 'mfanyakazi wa jua kali.'

Waziri Mkuu Odinga alidai kuwa Rais Kibaki anatekeleza maamuzi mhimu kama uteuzi wa mabalozi, maafisa wakuu wa serikali, na kwamba wakati mwingine amekuwa akipokea wakuu wa nchi za kigeni bila kumshirikisha au kuomba ushauri wake.

XS
SM
MD
LG