Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 20:46

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Auawa Burundi


Mwenyekiti wa OLUKOLE, Gabriel Rufili anasema mwanaharakati huyo wa kupambana na rushwa alichukuliwa kutoka nyumbani kwake na kuuawa. Aidha anasema watu waliohusika na uhalifu huo hawakuchukua kitu chochote mbali na nyaraka kadhaa alizokuwa nazo ndani.

Rufili anasema shirika lake linajishughulisha kwa kiasi kikubwa kupambana na rushwa iliyokithiri nchini humo, na kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa Manirumva aliuawa kwa sababu ya kazi yake ya kupambana na rushwa.

Maelezo hayo yameungwa mkono na Richard Ntawe wa shirika la kupambana na rushwa, Anti-Corruption and Economic Malpractice Observatory anasema mauaji ya Manirumva yanahusiana na kazi aliyokuwa akifanya.

Ntawe anasema Manirumva aliuawa kikatili kwa kuchomwa visu Alhamis asubuhi akiwa nyumbani kwake mjini Bujumbura.


Zinazohusiana

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG