Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 12:04

Waziri Mwingine Ang'atuka Kenya


Danson Mungatana alisema ameamua kujiunga na Bi.Karua kwasababu ya kutoridhika na mabadiliko na mageuzi yanavyoendeshwa ndani ya serikali ya mseto.Bw.Mungatana ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha Nak Kenya amesema wameshangazwa kwa kuwa walikuwa kwenye muungano ndani ya serikali wakimuunga mkono rais Kibaki lakini imeonekana kuwa rais amesahau kuyapa kipaumbele matatizo ya wananchi na ufisadi umezidi mno nchini humo.

Alisema msimamo wao nikwamba wangependa kuona mawaziri wote ambao wametajwa kuhusika na ufisadi wanachukuliwa hatua za kisheria kwani serikali imekuwa ikifumbia macho suala hilo, na shirika la kupambana na rushwa nchini Kenya halijachukua hatua yeyote hasa
kwa wale mawaziri waliotajwa kuhusika na rushwa.

Mawaziri hao bado wako serikalini na hawajafikishwa mahakamani. Badala yake alisema watu wadogo wadogo ndio wanaokamatwa. Aidha alisema serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kununua magari na kusahau suala la wakimbizi wa ndani na ufisadi ambao umekithiri.

Mungatana anasema msimamo wa chama cha Nak Kenya ni kwamba wangependa kuona watu hao wakifikishwa mahakamani na hatua zinachukuliwe dhidi yao. Alisema ni bora kwao kutokuwa katika uongozi wa serikali isiyowajibika kwa wananchi. Katibu huyu amefuata nyayo za kiongozi wa chama hicho Bi Martha Karua ambaye anajiandaa kugombea urais wa nchi hiyo 2012.XS
SM
MD
LG