Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 18:51

Martha Karua


Mtafaruku kati ya rais Mwai Kibaki na aliyekuwa Waziri wa sheria na masuala ya katiba Bi. Martha Karua umepelekea waziri huyo kujiuzulu akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu mjini Nairobi Bi. Martha Karua alisema "Leo hii nimemwandikia barua rais wetu barua ya kumjulisha ya kwamba nimeacha kazi kama waziri wake wa haki na masuala ya katiba na maridhiano kwa sababu nimeona siwezi nikaendelea kufanya hiyo kazi kama kwa maoni yangu nimezuliwa kufanya yale nimetumwa kufanya na siyo haki kuendelea kukaa kama nimezuiliwa kufanya hiyo kazi".Wachambuzi wa siasa za Kenya wanasema hali hiyo ilikuwa inatarajiwa wakati wowote kutokana na rais kumpa kisogo waziri huyo.

XS
SM
MD
LG