Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 07:29

Viongozi wa G-20 Kukutana Wiki Hii


Licha ya kwamba ni maarufu sana kwa watu wa Ulaya, Rais Barack Obama atakabiliwa na changamoto kubwa katika mkutano huo wa G-20, hususani kuhusu tatizo la kudorora kwa uchumi duniani.

Mjini London, Bwana Obama ataiwakilisha Marekani kwa mara ya kwanza katika jukwaa la kimataifa, wakati atakapokaa meza moja na wakuu wa nchi 20 zenye uchumi imara na zile zinazoinukia kiuchumi G-20.

Baadhi ya nchi zimelaumu mfumo wa Marekani ambapo masoko ya fedha yamepewa uhuru wa kuendesha shughuli zao bila usimamizi wa serikali na kusema ndio chanzo cha mgogoro huu wa uchumi duniani. Nchi nyingi zenye bajeti ndogo pia haziungi mkono sana matumizi makubwa ya serikali yanayoungwa mkono na Bwana Obama kama njia ya kuinua uchumi.

Maofisa wa juu wa White House wanasisitiza kuwa rais hana nia ya kushinikiza mataifa mengine kuhusu kiwango cha fedha wanachotakiwa kutumia.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG