Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 04:31

Spika wa Bunge la DRC Ajihuzulu


Uamuzi wa Spika wa Bunge, Vital Kamerhe kujihuzulu unafuatia wiki kadhaa za mvutano kati yake na serikali ya Congo, kuhusu uamuzi wa serikali ya nchi hiyo kukaribisha majeshi ya kigeni, kusaidia juhudi za kusambaratisha makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika, Salehe Mwanamilongo alisema kuwa Kamerhe alijihuzulu baada ya kupata shinikizo kali kutoka kwa viongozi mbalimbali nchini humo, na maelezo aliyoyatoa wakati wa hotuba yake kuwa asingependa jina lake liandikwe kwenye kitabu cha watu waliochangia kuleta ghasia nchini humo.

Mwanamilongo alisema kuwa huenda Spika wa Bunge Kamerhe alihofia kwamba kama ingefikia hatua ya wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, kuna uwezekano kuwa hatua hiyo ingeweza kuleta mpasuko wa kisiasa ndani ya chama chake, na hata katika taasisi nyingine za nchi hiyo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG