Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 14:50

Obama: Juhudi za Kimataifa Zinahitajika Kufufua Uchumi


Akizungumza Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari, Rais Barack Obama wa Marekani alisema dola ya Marekani iko imara kwasababu Marekani inauchumi imara kuliko mataifa mengine duniani.

Bwana Obama alisema kuwa atawaambia wajumbe wa mkutano wa G-20 mwezi ujao mjini London, kuwa mataifa yanatakiwa kufanya kila linalowezekana kuunda nafasi za kazi, na kusaidia uchumi kusonga mbele.

Kwa upande wa Marekani, Bwana Obama alisema kuwa ni muhimu kuingiza vita ya Afghanistan na Iraq katika bajeti ya Taifa, kwa sababu serikali haiwezi kuendelea na matumizi bila uwazi na ukweli. Alisema pia kuwa taifa lazima lifanye maamuzi magumu kupunguza nusu ya nakisi ya taifa ifikapo mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha uongozi wake.
XS
SM
MD
LG