Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 06:26

Utawala wa Obama na Mikakati Mipya ya Kufufua Uchumi


Utawala wa Rais Obama unasema mpango huo utasaidia kupata ufumbuzi wa tatizo la mikopo ambalo limevuruga uchumi wa Marekani. Bwana Obama anasema mpango huo utasaidia kufanya mikopo iendelee kutolewa.

Hata hivyo Bwana Obama ameonya kuwa mafanikio hayo hayatakuja mara moja, na kuongeza kuwa bado kuna udhaifu katika mfumo wa fedha, lakini kwamba wanafikiri kuwa wanaelekea katika mwelekeo ulio sahihi.

Mabenki mengi yamekuwa yakisita kutoa mikopo kwa kukosa uhakika kama kama watatakiwa kutumia fedha ya hazina kugharimia mabilioni ya dola yaliyotolewa kama mikopo. Rais Obama anasema programu hiyo mpya itakuwa ushirikiano kati ya serikali na wawekezaji binafsi.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG