Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 12:34

Majaji wa EAC  Wakutana Kigali


Mbali na lengo la kujadili kuhusu utawala bora, uhuru wa mahakama na ushindani katika mfumo wa siasa za vyama vingi, Jaji mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhani, amesema kuwa kulikuwa na haja pia kwa majaji hao kukutana kwa kuwa walikuwa hawajakutana tangu jumuiya hiyo ilipoundwa upya miaka 10 iliyopita.

Wajumbe wa mkutano huo wameashiria kuwa mswada huo utaungwa mkono kwa kiasi kikubwa kutokana na wajumbe kuridhika nao. Lakini bado utatakiwa kukubaliwa na hatimaye kuidhinishwa na viongozi wa kisiasa kutoka nchi wanachama.

Makamu mkuu wa Kenya, Emmanuel Okubasu anasema mkutano huo unamanufaa makubwa kwa sababu unawawezesha viongozi wa mahakama kupata ufumbuzi wa matatizo yanayo wakabili katika shughuli zao.

XS
SM
MD
LG