Licha ya juhudi alizofanya kuwapatanisha Rais Mwai Kibaki wa Kenya na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga ambaye sasa ni waziri mkuu wa nchi hiyo, Kofi Annan aliondoka Nairobi Jumatano kuelekea nchini kwake Ghana, bila kukutana na viongozi hao.
Hakuna kiongozi wa juu wa Kenya aliyekwenda kumpokea uwanja wa ndege wakati alipowasili akitokea kwenya mkutano mjini Dar es Salaam, Tanzania, na badala yake alilakiwa na waziri msaidizi.
Baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini Kenya, wamekasirishwa na madai kuwa Bwana Annan aliwaamuru Rais Kibaki na Waziri Mkuu Odinga, kwenda Geneva kwa mazungumzo yenye lengo la kujua hatma ya serikali ya mseto.
Muda mfupi baada ya kuwasili mjini Nairobi, Bwana Annan alisema wananchi wa Kenya wanahitaji uongozi imara, na kwamba makosa yanayofanyika hivi sasa nchini Kenya, yanasababishwa na viongozi kusahau matatizo yanayowakabili wananchi.
Bonyeza alama ya Sauti au Annan-Kenya kusikiliza ripoti kamili.