Baadhi ya viongozi wa makundi ya kutetea haki za binadamu walikamatwa jana mjini Kinshasa muda mfupi kabla ya kukutana na waandishi wa habari kwa lengo la kulalamikia mivutano ya kisiasa inayoendelea nchini humo.
Inaripotiwa makundi hayo yalikusudia kutoa taarifa yao kuhusu mvutano kati ya rais Joseph Kabila na spika wa bunge Vital Khamere siku moja kabla ya bunge kufunguliwa leo.
Wachambuzi wa kisiasa nchini Congo wanasema rais Kabila anaungwa mkono na wengi kwa sababu inaaminika amerejesha amani katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo. Kwenye mahojiano na Sauti ya Amerika machambuzi wa kisiasa Siad Ngonglutete kutoka Kinshasa amesema spika Khamere ameombwa na wabunge wengine ajiuzulu kwa madai kuwa anaenda kinyume na sera za chama chake. Lakini Khamere ana pinga msismamo huo akidai kwamba rais Kabila alichukua uwamuzi wa kukaribisha taifa la kigeni bila ya idhini ya bunge.