Mwana uchumi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha upinzani CUF nchini Tanzania, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa mkutano huo unatakiwa kujadili athari za mgogoro wa uchumi duniani kwa nchi za Afrika.
Profesa Lipumba amesema kuwa licha ya kwamba chanzo cha mgogoro huo ni katika nchi zilizoendelea kama Marekani, athari zake zinaonekana pia katika bara la Afrika. Amesema kuwa bei ya mazao yanayozalishwa katika bara hilo, imekuwa ikishuka kutokana na kupungua kwa mahitaji na matumizi ya mazao hayo katika soko la dunia.
Amesema kuwa biashara ya utalii imeathirika kutokana na mgogoro huo na hivyo kuzinyima nchi za Afrika mapato yatokanayo na biashara hiyo.