Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:12

AU Kuipigia Magoti UN Iahirishe Kukamatwa Bashir


Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika linasema limesikitishwa na kushindwa kwa Umoja wa Mataifa kuheshimu ombi la viongozi wa Afrika wanaotaka hati ya kukamatwa Rais Bashir iahirishwe.

Balozi Bruno Nongoma Zidouemba wa Burkina Faso ambaye anashikilia uenyekiti wa Baraza la Usalama la Afrika kwa wakati huu, anasema wanadiplomasia wa ngazi za juu kutoka Afrika, wanapelekwa New York kuwakilisha ombi hilo rasmi, na kuongeza kuwa anatumaini kuwa mpango huo utafanikiwa.

Akiongea Alhamis kwenye mkutano huo wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, Balozi wa Sudan, Mohieldin Salim Ahmed alisema kuwa hati hiyo itaathiri juhudi za kutafuta amani ya Darfur.

Kwa upande mwingine kuna hisia kuwa mahakama hiyo ya kimataifa inawalenga zaidi wahalifu kutoka Afrika, na kufumbia macho masuala yanayoendelea Mashariki ya Kati na mataifa yenye nguvu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.


XS
SM
MD
LG