Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 08:13

Kabila Akutana na Museveni


Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Museveni kutembelea DRC tangu majeshi yake yaliopoingia nchini humo kumuondoa madarakani Rais Mobutu Seseseko, hatua ambayo ilifuatiwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini DRC.

Mwandishi wa habari Ruben Lukumbuka anaripoti kutoka mashariki mwa Congo kuwa wananchi wa eneo hilo walisubiri kwa hamu kubwa kukutana na rais wao ambaye anatembelea mashariki mwa Congo kutathmini hali ya maisha kwa wakazi wa eneo hilo.

Marais hao wawili walijadili pia kuhusu uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili miaka kadhaa baada ya uhasama uliofuatia mapigano nchini DRC yaliyohusisha majeshi ya Uganda na mataifa mengine jirani .

Mkutano huu kati ya marais Kabila na Museveni huenda ukafungua ukurasa mpya wa uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili ambazo zimekuwa na uhasama wa muda mrefu ambao baadhi ya wachambuzi wanaamini kwamba umeathiri hali ya kisiasa na kiuchumi katika eneo hilo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG