Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 17, 2025 Local time: 19:03

Rais wa Guinea-Bissau Auawa


Uamuzi huo unafuatia mkutano wa mawaziri ambao wanataka waendesha mashitaka kuchunguza mauaji hayo ya rais na mkuu wa majeshi Tagme Na Waie ambaye aliuawa Jumapili katika tukio tofauti la mlipuko wa bomu.

Hakuna mtu au kundi la watu waliodai kuhusika na mauwaji hayo, lakini vyanzo vya usalama vinasema Bwana Vieira alipigwa risasi na kuuawa na wanajeshi waasi, ambao huenda walikuwa wakilipiza kisasi kwa kifo cha mkuu wa majeshi.

Jeshi limekanusha kuhusika na mauaji ya rais. Msemaji wa jeshi anasema shambulio hilo lilifanywa na kundi tofauti kabisa, na kusisitiza kuwa jeshi halifanyi jaribio la kufanya mapinduzi.

Awali jeshi lilitoa taarifa na kusema kuwa litaheshimu utaratibu wa katiba na demokrasia katika nchi hiyo ya Afrika magharibi. Katiba ya nchi hiyo inataka Spika wa bunge la nchi hiyo Raimundo Perreira kuchukua madaraka hadi pale uchaguzi utakapokuwa umefanyika katika kipindi cha siku 60.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG