Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:10

Serikali ya Kenya Yazidi Kubanwa


Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yamefanya maandamano mjini Nairobi, yakimtaka Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, Philip Alston anayechunguza mauwaji hayo.

Mashirika hayo yanataka watu waliotajwa katika ripoti hiyo ya Profesa Alston waachishwe kazi mara moja, na kudai kuwa ikiwa serikali itashindwa kuwaondoa kwenye nafasi hizo, basi wananchi watachukua jukumu hilo na kuwaondoa ofisini.

Serikali ya Kenya haijatoa maelezo rasmi kuhusu mapendekezo hayo, lakini maafisa wa idara maalum ya usalama wa taifa, wamepinga vikali ripoti hiyo na baadhi yao wamekuwa wakifanya kazi yao kwa taratibu mno. Bonyeza alama ya sauti au Mauwaji Kenya hapo juu kusikiliza ripoti kamili.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG