Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 08:07

UN Yashutumu Jeshi la Polisi Kenya


Serikali ya Kenya pia imegawanyika kuhusu ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa, na kunawasiwasi kama Rais rais wa Nchi hiyo Mwai Kibaki atakubali kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti hiyo.

Ripoti ya mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauwaji hayo yanayodhaniwa kufanywa na maofisa wa polisi, imezua hisia tofauti miongoni mwa wananchi wa kawaida, viongozi wa serikali, na mabalozi na wanasiasa kwa ujumla.

Muda mfupi baada ya mjumbe huyo kuwasilisha ripoti hiyo, msemaji wa serikali, Dokta Alfred Mutua, ametoa taarifa kali ya kukanusha madai ya ripoti hiyo kuhusu ukatili unaofanywa na maofisa wa polisi dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia. Bonyeza alama ya sauti au UN-Kenya kusikiliza ripoti kamili.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG