Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 20:00

Warundi Waomboleza Vifo Vya Wanajeshi Wao Somallia


Wananchi wa Burundi wamepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuuwawa wanajeshi wao katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika, AMISOM nchini Somalia.

Kambi ya kikosi hicho mjini Mogadishu ilishambuliwa na wajitoa mhanga siku ya jumapili na kusababisha vifo vya wanajeshi 11 wa Burundi. Wanajeshi wengine 15 walijeruhiwa.

Hiyo jana Umoja wa Afrika umesema utaendelea na juhudi zake za kuleta amani huko Somalia na mataifa mawili yeneye majeshi yake huko, Uganda na Burundi yameahidi kutofanya mabadiliko yeyote.

Innocent Muhozi, mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Burundi, anasema wanajeshi wa kulinda amani nchini Somalia ni wachache na hawana mafunzo na vifaa vya kutosha kukabiliana na waasi wa nchi hiyo.

Muhozi amesema kuna haja kwa bara la Afrika kuongeza juhudi zake za kupata ufumbuzi wa matatizo ya Somalia, akisema kushindwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha madhara makubwa siku zijazo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG