Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 06:31

Obama Atembelea Canada


Ziara hiyo ya Rais Barack Obama ni ya kwanza nchi za nje tangu aliposhinda uchaguzi wa rais na kuingia White House Januari 20 mwaka 2009. Kiutamaduni ziara ya kwanza ya rais mpya wa Marekani nje ya nchi inakuwa Canada, nchi jirani yenye uhusiano wa karibu na wa muda mrefu na Marekani. Rais Obama na Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper, walijadili miongoni mwa mambo mengine, kuhusu namna ya kukabiliana na mgogoro wa uchumi duniani.

Waziri Mkuu Harper alisema yeye na Bwana Obama walikubaliana Alhamis kuwa Canada na Marekani lazima washirikiane kukabiliana na kuzorota kwa uchumi duniani.

Alisema kuwa walikubaliana kuchukua hatua muhimu na za haraka kukuza uchumi tena, na kuwalinda wafanyakazi na familia ambazo zimeathiriwa vibaya na kudorora kwa uchumi.


XS
SM
MD
LG