Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:35

Waziri Ruto Aponea Chupuchupu


Baada ya mjadala mkali katika bunge, baadhi ya wabunge wa Kenya walipinga vikali kuondolewa kwa Waziri wa Kilimo wa Kenya, William Ruto kwenye baraza la mawaziri. Wabunge 119 walipinga kuondolewa kwake, na hivyo kuwazidi nguvu wabunge 22 waliopiga kura kutaka aondolewe.

Watetezi wa hoja hiyo iliyowakilishwa bungeni kwa lengo la kumwondoa Bwana Ruto kwenye nafasi ya uwaziri wa kilimo, walidai kuwa yeye kama waziri, alitakiwa kuwajibishwa kutokana na tatizo la mahindi kuendelea chini ya usimamizi wake.

Lakini Waziri Ruto aliliambia bunge kuwa hastahili kulaumiwa kwa matatizo hayo ya chakula nchini Kenya, kwa maelezo kuwa ofisi yake inahabari za kuaminika kuwa tatizo la chakula linaukumba ulimwengu mzima, na siyo Kenya peke yake.

Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga hakuhudhulia mjadala huo, na haijulikani wazi anamaoni gani kuhusu swala hilo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG