Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:14

Kamanda Asema Operesheni ya DRC Yafanikiwa


Kiasi cha mwezi mmoja tangu operesheni ya pamoja ya majeshi ya DRC na Rwanda kuanza mashariki mwa DRC kuwang'oa waasi wa Rwanda wa FDLR, kiongozi wa kikosi hicho Jenerali John Numbi anasema waasi wa FDLR wameng'olewa katika maeneo mengi waliyokuwa wakiyashikilia katika maeneo ya Kivu Kaskazini na Kusini.

Jenerali Numbi anasema wananchi wa maeneo hayo hivi sasa wameanza kutembea kwa huru katika majimbo hayo, ikiwa ni ishara kuwa hali ya usalama inaanza kurudi katika maeneo hayo. Jenerali huyo anasema operesheni hiyo inaendelea kuwasaka waasi wa FDLR na kuwatia nguvuni, kuwarejesha nchini Rwanda.

Jenerali Numbi pia alisema kuwa wanajeshi wa Rwanda wataondoka nchini DRC mwishoni mwa mwezi Februari kama ilivyokubaliwa kati ya nchi hizo mbili kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo. Jenerali Numbi pia alikanusha madai kuwa wanajeshi katika operesheni hiyo wamekuwa wakikiuka haki za raia.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG