Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 06:53

Museveni Abadili Mawaziri


Rais Yoweri Museven wa Uganda amemfuta kazi Waziri wa Fedha katika mabadiliko ya baraza la mawaziri ambayo yanatoa nafasi mpya kwa mke wake na kaka yake. Ofisi ya rais imetangaza leo kuwa waziri wa zamani wa nishati Sydda Bbumba atachukua nafasi ya Ezra Suruma kama Waziri wa Fedha.

Taarifa hiyo inasema Suruma ataendelea kuwa mshauri wa rais katika masuala ya fedha. Rais alimteuwa mke wake, Janet Museveni kama waziri wa jimbo la Karamoja kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Mchambuzi wa siasa nchini Uganda, Don Wanyama anasema uteuzi wa Janet kuwa mmoja wa mawaziri wa nchi hiyo ni hatua muhimu katika juhudi za kuwasaidia watu wenye shida. Bwana Museven alimtaja pia kaka yake, Salim Saleh kuwa mshauri mpya wa maswala ya ulinzi. Mwaka uliopita Bwana Museveni alimteuwa mwanae, Muhoozi Kainegugaba kuwa kamanda wa jeshi maalum.

XS
SM
MD
LG