Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:20

Burundi Yaunda Tume ya Kusimamia Uchaguzi


Wajumbe hao watano walipendekezwa na Rais Pierre Nkurunziza kuwa wanachama wa tume huru ya kusimamia uchaguzi utakaofanyika nchini humo mwaka 2010.

Miongoni mwa wajumbe hao watano, watatu wanatoka chama tawala CNDD-FDD, UPRONA na Frodebu, na wajumbe wawili waliosalia wanatoka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs).

Wiki mbili kabla ya uamuzi huu wa sasa wa Bunge, Rais Nkurunziza aliteuwa wajumbe ambao walipingwa na hawakuidhinishwa na bunge.

Domisire Ndayizeye, gombea wa kiti cha urais katika uchaguzi huo wa mwaka 2010, amekaribisha uteuzi wa wajumbe hao na kusema ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa wakati wa mashauriano kati ya Serikali na vyama vinavyowakilishwa bungeni.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG