Mchambuzi wa siasa, Dokta PLO Lumumba anasema miongoni mwa sababu zilizowafanya wabunge kuukataa mswada ambao ungewezesha kuundwa kwa mahakama maalum ya kuwashitaki watuhumiwa wa machafuko hayo, ni kuhakikisha sheria inawashughulikia watuhumiwa bila kuwapa nafasi ya kuipatia hongo mahakama ya Kenya.
Tayari Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan ambaye pia alikuwa msuluhish wa mgogoro wa kisiasa wa Kenya, ameomba apewe majina ya washukiwa viongozi ili aweze kuyakabidhi kwa mahakama ya kimataifa mjini The Hague.
Lakini Dokta Lumumba anasema kama Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga wakiomba na kutoa maelezo ya kina, wanaweza kupewa nafasi zaidi ya kurejesha mswada huo uliotupiliwa mbali na bunge la Kenya ili kupigiwa kura tena.