Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:48

MV Faina Yawasili Mombasa


Meli kubwa ya Ukraine MV Faina hatimaye imewasili katika bandari ya Kilindini, Mombasa Kenya chini ya ulinzi mkali, huku mamia ya waandishi habari wa kimataifa na wale wa Kenya pamoja na umati mkubwa wa watu wakishuhudia kuwasili kwake.

Akizungumza na sauti ya Amerika kutoka bandarini mara tu baada ya kuwasili meli hiyo, Josephat Kioko mtangazaji wa Radioya Baraka FM ya Mombasa, alisema kwamba MV Faina,iliwasili alasiri alhamis ikiwa inapeperusha bendara kadhaa mojawapo ikiwa bendera ya taifa la Kenya.

Maharamia wa Somalia walikuwa wameiteka nyara meli hiyo lakini wakaiachia baada ya kulipwa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 250. Bwana Kioko aliieleza sauti ya Amerika kuwa serikali ya Kenya imesema rasmi kuwa silaha nzito zilizobebwa katika meli hiyo ni za Kenya.Hapo awali kulikuwa na mashaka ikiwa silaha hizo zilizotengenezewa Russia ni mali ya Kenya au ya Sudan.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG