Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:24

Bunge Kenya Lakataa Mswada wa Mahakama Maalum


Bunge la Kenya limekataa kupitisha mswada wa kuundwa mahakama maalum ambayo ingesikiliza kesi za washukiwa wa mauwaji na uhalifu mwingine uliofanyika wakati wa ghasia zilizofuatia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo Disemba 2007.

Kushindwa kwa mswada huo ni pigo kubwa kwa serikali ya Kenya ambayo imekuwa ikisisitiza kuwa watuhumiwa wa machafuko hayo wanatakiwa kushitakiwa na mahakama ya nchi hiyo.

Mswada huo umeshindwa licha ya Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga, kufanya kampeni kuwashawishi wabunge waupigie kura ya ndiyo mswada huo.

Akiongea na wabunge wenzake kabla ya mswada huo kupigiwa kura, mbunge wa ODM Kenya Bwana Johnson Mudhama, amesema sasa washukiwa watapelekwa mahakama ya kimataifa ICC mjini The Hegue ambapo watafunguliwa mashitaka ya mauwaji.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG