Upatikanaji viungo

Ntaganda: Sina Sababu ya Kuogopa

  • Salehe Mwanamilongo

Kiongozi wa waasi wa CNDP ambao wamekuwa wakipambana na majeshi ya serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema hana sababu ya kuogopa kukamatwa kwa sababu hajafanya kosa.

Akiongea na Sauti ya Amerika, Jenerali Bosco Ntaganda amesema yeye na kundi lake waligundua kuwa mapigano yaliyokuwa yakiendelea kati ya kundi lake na serikali ya Congo hayakuwa na manufaa, na ndiyo sababu wameamua kuweka silaha chini na kushirikiana na serikali.

Chini ya makubaliano ya sasa, Jenerali Ntaganda ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa kwa tuhuma za uhalifu wa kivita, atakuwa na cheo kikubwa katika jeshi la taifa. Bonyeza alama ya Sauti au DRC Ntaganda kusikiliza mahojiano kamili.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG