Nchini Uganda chama cha upinzani kinachoongozwa na bwana Kizza Besigye kimesema kinafanya mabadiliko ya uongozi kuanzia mashinani ili kujiandaa kwa uchaguzi wa urais mwaka wa 2011.
Lakini kuna ripoti kuwa chama hicho Forum for Democratic Change au FDC kimegubikwa na mzozo wa ndani kwa ndani. Bwana Besigye anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Meja Jenerali Mugisha Muntu na wanachama wengine wa chama chake.
Akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Kampala, Besigye alisema chama hicho kimeamua kufanya marekebisho ya uongozi na kwamba anatumaini ataendelea kuwa rais wa chama, huku chama kikijiandaa kwa uchaguzi wa uaris hapo mwaka 2011.
Katika mahojiano hayo, bwana Besigye pia alisema ataendelea kupigania haki za waganda na kupinga utawala Rais Yoweri Musebeni, ili waganda wajikwamue kutokana na uongozi wake wa zaidi ya miongo miwili.