Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 05:01

UN: Hali ya Kibinadamu DRC Bado ya Wasiwasi


Umoja wa Mataifa unasema hali ya kibinadamu kwa watu waliolazimishwa kuyakimbia makazi yao kutokana na vita kati ya majeshi ya serikali na waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado ni ya wasiwasi.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na masuala ya kibinadamu, John Holmes anaendelea na ziara yake ya kuwatembelea watu wanaoishi katika makambi ya wakimbizi kwa lengo la kujua matatizo na na mahitaji waliyonayo.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika, Salehe Mwanamilongo ambaye ameambatana na msafara wa bwana Holmes, amesema kuwa wakimbizi hao wamemwambia Holmes kuwa wangependa kurudi makwao, lakini bado wanawasiwa kuwa huenda waasi wa LRA wakawashambulia kulipiza kisasi baada ya kushambuliwa na majeshi ya pamoja kutoka DRC, Uganda na Sudan Kusini.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG