Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:26

Kashfa ya Mahindi Kenya, Lucy Kibaki Ahusishwa


Wakenya wanakabiliwa na baa la njaa huku kukiwa na madai kuwa baadhi ya wanasiasa na watu mashuhuri wanahusika na ufisadi wa kuuza mahindi kutoka ghala ya taifa kwa manufaa yao binafsi.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika, Ababu Namwamba ambaye ni mbunge wa Budalangi nchini Kenya, alisema Jumatano kuwa kuna 'uvumi' kwamba baadhi ya makampuni yamekuwa yakinunua na kuuza mahindi kutoka ghara ya taifa kwa njia isiyokuwa halali.

Mheshimiwa Namwamba alisema kuwa wiki mbili zilizopita waziri wa kilimo wa Kenya, William Ruto aliwasilisha bungeni orodha ya makampuni 600 ambayo yanadhaniwa kuhusika na biashara hiyo haramu.

Namwamba alisema kuwa aliwasilisha majina ya wakurugenzi wa makampuni hayo, na miongoni mwa majina hayo ni Lucy Kibaki ambaye ni mke wa Rais Mwai Kibaki wa Kenya.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG