Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:50

Ajali Nyingine Kenya, Watu Waenda Tena Kuchota Mafuta


Wakati wakenya wakiendelea kuomboleza vifo vya watu waliokufa kwa ajali mbili tofauti za moto, ajali nyingine imetokea eneo la Naivasha, na kama ilivyokuwa kwa tenka la mafuta ambalo liliripuka na kuuwa idadi kubwa ya watu, watu wa eneo hilo walikimbilia eneo la ajali kuzoa mafuta kutoka gari ya moshi ambayo iliacha njia.

Polisi walikuwa na kazi ngumu kuwazuwia wakazi wa eneo hilo, waliokuwa wakijaribu kuchota mafuta kutoka eneo hilo. Lakini mbali na matukio hayo mawili ya kusikitisha ambapo watu wasiopungua 140 wamekufa, mzozo mpya umeanza kujitokeza nchini Kenya kati ya mke wa Rais Mwai Kibaki, Lucy Kibaki na baadhi ya mawaziri na maofisa wakuu katika serikali.

Kwa habari zaidi, sikiliza ripoti kamili ya mwandishi wetu wa Nairobi, Mwai Gikonyo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG