Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:10

Mauritania, Guinea Wazuiliwa Mkutano wa AU


Umoja wa Africa umewazuwia wajumbe kutoka Mauritania na Guinea kuhudhuria mkutano kwa maelezo kuwa mapinduzi ya kijeshi katika nchi hizo yamewaondolea sifa ya uanachama katika umoja huo.

Mwenyekiti wa tume ya kiutendaji ya AU, Bernard Membe ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, alisimama Alhamis wakati wa ufunguzi wa mkutano wa awali wa mawaziri, na kutangaza kuwa wajumbe kutoka Mauritania na Guinea wamekatazwa kuhudhuria.

Membe aliwaomba wajumbe wengine wa AU kuwataarifu wajumbe wa Guinea na Mauritania kuwa mapinduzi ya kijeshi ambayo awali yalikuwa kitu cha kawaida katika bara la Afrika hayatavumiliwa tena.

Katika hotuba kali ya kuadhimisha mwaka mmoja wa uenyekiti wa Tanzania katika umoja huo, Membe aliweka wazi kuwa shirika hilo la Afrika, linapinga hatua yoyote ya mahakama ya kimataifa ICC kumfungulia mashtaka Rais Omar al-Bashir wa Sudan.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG