Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:44

UN: Hali ya Kibinadamu DRC Inatia Wasiwasi


Mkuu wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, Navi Pillay anasema hali ya kibinadamu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatia wasiwasi, na kuwataka wahusika wote katika mgogoro wa eneo hilo kuheshimu haki za binadamu na sheria za kimataifa.

Pillay anasema kundi la waasi wa Uganda Lord's Resistance Army (LRA) linafanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa kushambulia vijiji mashariki mwa Congo na kuwatisha raia tangu pale lilipohamishia makazi yake katika eneo hilo likitokea Sudan.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Rupert Collville anasema Kamishna Pillay hapingi oparesheni za kijeshi dhidiya LRA, lakini anawasiwasi kwa sababu rekodi za siku za nyuma zinaonesha kuwa oparesheni za majeshi ya serikali zilisababisha matatizo makubwa kwa raia.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa LRA imeuwa raia 500 na kuwalazimisha wengine zaidi ya laki moja kuyakimbia makazi yao.


Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG