Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 15:07

Al-Shabab Waiingia Baidoa


Kundi la wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia limechukua udhibiti wa mji wa Baidoa ambao ni makao makuu ya bunge la nchi hiyo. Mashahidi wanasema al-Shabab waliteka mji huo Jumatatu, saa chache baada ya majeshi ya Ethiopia waliokuwa wakiunga mkono serikali ya mpito ya Somalia kumaliza kuondoa wanajeshi wake kutoka mjini humo na katika Somalia nzima.

Wakazi waliripoti mapigano makali kabla ya mji huo kutekwa. Hakuna maelezo yoyote kuhusu vifo au majeruhi. Idadi kubwa ya wabunge wa Somalia hivi sasa wako katika nchi jirani ya Djibouti kwa ajili ya kikao maalum cha bunge kilichoanza Jumapili.

Jumatatu, wabunge hao walipiga kura kuongeza mara mbili ukubwa wa bunge hadi kufikia wajumbe 550, kama ilivyokubaliwa katika mapatano ya amani kati ya serikali na waislamu wenye sera za kadiri mwezi Oktoba.

XS
SM
MD
LG