Ethiopia inasema imekamilisha zoezi la kuondoa wanajeshi wake walioingia Somalia miaka miwili iliyopita kuondoa wapiganaji wa kiislamu na kuiwezesha serikali ya mpito nchini humo kurejea madarakani.
Waziri wa mawasiliano wa Ethiopia, Bereket Simon amesema kikosi cha mwisho cha wanajeshi 3000 wa Ethiopia waliokuwa Somalia wamerudi nyumbani.
Kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa Ethiopia, jukumu la usalama nchini Somalia limebaki mikononi mwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrikja (AMISOM), chenye wanajeshi 3,400 na wanajeshi wengine 10,000 wa serikali.
AMISOM inaupungufu wa wanajeshi 8,000 na hivyo kuzidisha wasiwasi kuwa kuondoka kwa majeshi ya Ethiopia kunaweza kupelekea hali mbaya zaidi ya usalama nchini Somalia.