Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 03:19

Nkunda Akamatwa na Jeshi la Rwanda


Kiongozi wa waasi huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Laurent Nkunda amekamatwa na jeshi la Rwanda baada ya kujaribu kukwepa kukamatwa na jeshi la Congo.

Akizungumza na sauti ya Amerika Gavana wa jimbo la Kivu ya Kaskazini Julien Paluku amesema Nkunda alikimbilia Rwanda baada ya kujaribu kupambana na jeshi la DRC kutokana na kuingia majeshi ya Rwanda huko Congo.

Hivi karibuni Nkunda alikanusha kwamba ameondolewa kutoka uwongozi wa kundi la waasi la CNDP, baada ya kuripotiwa mgawanyiko katika kundi hilo la waasi. Wachambuzi wanasema alikua pia kipingamizi kikuu katika kufikia makubaliano ya kuleta amani katika eneo hilo la mashariki ya Congo.

Gavana Paluku anasema kukamatwa kwake kunaleta matumaini makubwa ya kupatikana amani katika jimbo lake. Na kwamba wananchi wamefurahia sana kukamatwa kwa Nkunda. Alisema hivi sasa majadiliano yatafanyika kati ya serekali za Kigali na Kinshasa juu ya namna ya kumrudisha huko DRC. Hakuna mashtaka ya kimataifa dhidi yake kwa wakati huu.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG