Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 21:55

Safari ya Obama Kuelekea White House


Safari ya Barack Obama kuelekea White House ilikuwa ndefu, ngumu na yenye machungu mengi kwake yeye binafsi, na kwa taifa zima la Marekani, hususan wamarekani weusi ambao walipelekwa Marekani kwa nguvu kama watumwa, na wamarekani weupe ambao mwaka jana walilazimika kuweka kando hisia zao za kibaguzi na kumpigia kura Obama.

Rais Obama ameingia Ikulu miaka 45 tu tangu sheria za ubaguzi wa rangi kupigwa marufuku kufuatia harakati za mapambano ya kupigania haki za watu wa rangi zote katika miaka ya 1960.

Harakati za kupambana na utumwa zilianza karne ya 19 na baadaye mapambano ya kupigania haki za kiraia katika karne ya 20.

Katika harakati hizo ubaguzi wa rangi ulivunjwa hatua kwa hatua, na mwishoni mwa miaka ya 1950 na mwanzoni mwa maiaka ya 1960, harakati hizo zilichukua sura mpya kwa kuongozwa na kiongozi shupatu wa kutetea haki za binadamu, Dokta Martin Luther King Jr.

Kuingia kwa Rais Obama White House ni matunda ya kazi ngumu na yenye machungu mengi iliyofanywa na wamarekani weusi na baadhi ya wazungu kupigania haki za watu weusi ambao walikuwa wakishikiliwa kama watumwa.

XS
SM
MD
LG