Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 16:19

Rais Obama Kufunga Guantanamo Bay


Rais Barack Obama wa Marekani anakusudia kusitisha kesi zinazo wakabili washukiwa wa ugaidi wanaoshikiliwa katika gereza la Marekani nchini Cuba, Guantanamo Bay ikiwa ni moja ya hatua zake za mwanzo kuchukua kama rais.

Jumanne jioni wakati watu walipokuwa katika tafrija mbalimbali kusherehekea kuapishwa kwake, Rais Obama na Waziri wa Ulinzi Robert Gates walikubaliana kuwasilisha amri ya kusimamisha kesi za Guantanamo kwa siku 120.

Kusitishwa kwa utaratibu huo kutaupa utawala wa Obama nafasi ya kutathimini utaratibu mzima wa mahakama ya kijeshi ya Guantanamo, ambao umekuwa ukikosolewa sana na makundi ya kutetea haki za binadamu.

Bwana Obama aliashiria katika hotuba yake baada ya kuapishwa kwamba ana mpango wa kuchukua mwelekeo mpya kwa sera za mambo ya nje za marekani. Jumatano alikutana na washauri wa juu wa usalama na kijeshi kufanya tathimini upya ya vita ya Iraq na Afghanistan.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG