Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 16:05

Barack Obama Rais Mpya wa Marekani


Baada ya miaka miwili ya kampeni kali, siku 78 za utawala wa mpito na sherehe za kukabidhiwa madaraka Rais Mpya wa Marekani Barack Obama ananaza siku yake ya kwanza kwa kushughulikia masuala ya kigeni.

Katika hotuba yake ya kwanza akiwa kiongozi wa 44 wa taifa hili kuu la dunia siku ya Jumanne, Rais Obama alisema "na mfahamu kwamba Marekani ni rafiki wa kila taifa, na kila mwanamume, mwanamke, na mtoto wanaotaka mustakbali wa amani na kuheshimiwa hadhi yao. Basi sisi tuko tayari kuongoza kwa mara nyingine."

Washauri wa rais wanasema hatua ya kwanza ya rais mpya ni kumteua Bw George Mitcheln kua mjumbe wake wa Mashariki ya Kati. wakati wa utawala wa mpito Bw Obama alikosolewa kwa kuka kimya kutokana na uvamizi wa Israel huko Gaza.

Baadae hii Jumatano inaripotiwa kwamba huwenda rais akakutana na washauri wake wa usalama wa kitaifa kutafakari juu ya vita vya Irak na Afghanistan. Na inaripotiwa huwenda akakutana pia na washauri wake wa masuala ya kiuchumi kuzungumzia mzozo wa kiuchumi wa nchi hii.


XS
SM
MD
LG