Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:56

Mogadishu Baada ya Majeshi ya Ethiopia Kuondoka


Kundi la mwisho la wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wamebaki Somalia limeondoka Alhamis na kupelekea hali ya wasiwasi miongoni mwa wananchi wa Somalia kuwa hatua hiyo huenda ikafuatiwa na machafuko zaidi.

Tayari matatizo mbalimbali ya kiusalama yameanza kujitokeza nchini humo na wanamgambo wa kiislamu wameanza kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na yaliyokuwa makao rasmi ya kiongozi wa nchi hiyo.

Waziri Mkuu Nur Hassan Hussein, anasema wanajeshi kadhaa kutoka Umoja wa Afrika bado wako nchini Somalia, lakini sehemu kubwa ya nchi hiyo inadhibitiwa na wanamgambo wa kiislamu.

Mwakilishi maalumu wa Somalia katika Umoja wa Mataifa ameomba jumuiya ya kimataifa kujihusisha zaidi na matatizo ya Somalia baada ya majeshi ya Ethiopia kuondoka mji mkuu Mogadishu.


XS
SM
MD
LG