Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 06:15

Kuapishwa kwa Obama


Barack Obama ataapishwa kama Rais wa 44 wa Marekani Januari 20, na kuendeleza utamaduni wa kukabidhiana madaraka kutoka kwa kiongozi mmoja hadi mwingine, utaratibu ambao ulianzia mwaka 1789 wakati alipoapishwa George Washington.

Akiwa rais wa kwanza mmarekani mwenye asili ya Afrika, Barack Obama anaona kuna jambo linalofanana na rais wa 16 wa taifa hilo, Abraham Lincoln, shujaa wa wamarekani wengi weusi kwa uongozi wake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bwana Obama atatoa heshima kwa Lincoln atakapokula kiapo cha kuchukua madaraka, huku akiwa ameuweka mkono wake kwenye biblia ambayo lincloln aliitumia wakati alipoapishwa mwaka 1861.

Marvin Kranza, mtaalamu katika masuala ya sherehe za kiapo anasema, "Hili ni moja ya matukio muhimu sana ambayo tunaweza kuyaita dini ya kiraia humu nchini."

Kuapishwa kwa rais mpya kunahitajika kwa mujibu wa katiba na zoezi la kula kiapo linasimamiwa na jaji mkuu wa Marekani. Kiapo hicho kinamuweka madarakani rais mpya kutoa ahadi ya kweli ya kuchukua madaraka na kuihifadhi, kuilinda na kuitetea katiba.


Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG