Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 08:45

Jenerali Nkunda Ang'olewa Madarakani?


Kundi la waasi wa CNDP mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, linadai kuwa limemwondoa kwenye nafasi ya uongozi wa kundi hilo, Jenerali Laurent Nkunda na kutangaza uongozi mpya.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Jumanne, Desire Kamanzi, aliyejitaja kama Mkuu wa Kamati ya Siasa inayotathmini hali ya baadaye ya CNDP amesema Jenerali Nkunda sio tena kiongozi wa CNDP.

Kamanzi amesema, "Tangu Januari nne, Jenerali Nkunda siyo kiongozi tena CNDP," na kuongeza kuwa kuna tuhuma nyingi dhidi yake, miongoni mwa hizo ni uongozi mbaya, kuchelewesha makubaliano ya amani yanayoendelea Nairobi, na kuingia mikataba mibovu na serikali ya China.

Licha ya kwamba Jenerali Nkunda alikanusha siku chache zilizopita madai ya kuondolewa kwake, Kamanzi amesema hana mamlaka tena na kwamba uongozi mpya utachunguza kuona kama kuna haja ya kumchukulia hatua za kinidhamu. Matamshi ya Kamanzi hayakuweza kuthibitishwa na pande huru ndani ya DRC.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG