Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 07:05

DRC: Mahojiano na Jenerali Nkunda


Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, ambaye pia ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amewasili nchini humo ambapo anatazamiwa kukutana na rais Joseph Kabila, na kiongozi wa kundi la waasi wa CNDP, jenerali Laurent Nkunda.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika kutoka mji wa Bunagana Alhamis, Jenerali Nkunda alisema anategemea kuwa mazungumzo baina yake na bwana Obasanjo yatampa uelewa zaidi mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa, kuhusu mtafaruku wa Congo.

Jenerali huyo alisema pindi wapatanishi wa mzozo wa Congo watakapo uelewa mtafaruku huo, wataweza kutanzua vyema maswala yanayozungumziwa katika mkutano unaoendelea mjini Nairobi nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG