Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 03:54

Matumaini ya Waafrika kwa Obama


Watu kote duniani wanasubiri kwa hamu kubwa kuapishwa kwa Barack Obama kama rais wa Marekani, huku kukiwa na matumaini kuwa huenda ataweza kuleta mabadiliko duniani.

Matumaini ni makubwa zaidi kwa bara la Afrika ambapo kuna mizizi ya bwana Obama. Hili lilikuwa wazi pale mamilioni ya waafrika alipokaa macho usiku mzima kama ilivyokuwa Marekani, wakisubili kushangilia kutangazwa kwa Barack Obama kama rais ajaye wa Marekani.

Profesa Veroniqe Tadjo wa chuo kikuu cha Witwatersrand mjini Johannesburg, anasema kwa watu wenye asili ya Afrika ulikuwa ni wakati wa furaha kubwa na wakihistoria.

Tadjo anasema Obama ameleta matumaini makubwa na kwamba amebadili mambo mengi kwa watu wengi kuhusu namna wanavyo jitizama. Anasema, "Mtu mweusi kuwa mtu mwenye nguvu kuliko wote duniani ni kitu muhimu sana."

Lakini Francis Kornegay, mmarekani mweusi na mtafiti aliyeishi katika bara hilo kwa miaka 13, anasema baadhi ya waafrika wanaonya watu wenye matumaini kupita kiasi na urais wa Obama.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG